Salam Kaka Michuzi na Watanzania wote
 Naomba niwekee hizi picha nne za Watanzania wawili waliojeruhiwa vibaya na kikundi cha watu wapatao 20 hadi sasa haijajulikana ni akina nani kama ni Waalbania au Ni vishoka wengine au Wagiriki. Tukio limetokea jana usiku wakati walipopita karibu na watu hao waliowajeruhi ambao wanasema walikuwa wamevunja gari za watu kuiba sasa inaonekana kuwa walifikiria wataita polisi ndipo walipowavamia
 Ahsante - Mdau Ugiriki




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Hee poleni lakin rudini nyumbani au angalieni usawa mwingine! Huko inaonekana manapata shida sana! Hakuna palipo pazuri hata kama ni nyumbani lakini kuna ubora wake kuwa kwenu! Ukiend US nao wanatungua watu weusi kama kunguru! japo sio mara zote!

    ReplyDelete
  2. poleni sana wanangu vp tena...? au mambo ya mauzo hayo uzito mmbovu. no matter what...! don't lose hope nigga.

    ReplyDelete
  3. Poleni watanzania....rudini nyumbania kubaya huko!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Mungu wangu! Poleni sana. Mie nilikuwa Rhodes (Kiotari) kwa wiki mbili likizo ila sikuona haya. Labda kwa kuwa kule ni vijijini. Bahati mbaya ngozi ni wa kuonewa hata kwao, hivyo kurudi nyumbani sio solution, kwani najua kesi za kusingiziwa hapo Tandale na nusu kuchomwa mtu kwa kilio cha wizi. Hapa nilipo wao wanaua jumla na video kuweka youtube. Nawatakia mpone mapema. Blackmpingo

    ReplyDelete
  5. Hakuna mahali ambapo ni salama 100%duniani. Mbona hata nyumbani baadhi ya watu wanamwagiwa tindikali, wanatobolewa macho, wanan'golewa meno, wanauwawa kwa tuhuma za kishirikina, the list goes on and on. Tafsiri ya neno "nyumbani" siyo "salama"

    ReplyDelete
  6. naungana na wote pia kasoro wa mwanzo na wa pili Kurudi home sio solution sina haja ya kurudia Ila langu ni HILI

    WALE WAUZA UNGA WALOKAMATWA SOUTH AFRICA NA WALEE WA HONGKONG MBONA SERIKALI IMEKUWA IKISHUHULIKA NAO SANA AU KWA KUWA NI MASTAA ?

    HIVI HAWA NDUGU ZETU WA KIGIRIKI KUNA LOLOTE LINAFANYWA NA BALOZI WA TANZANIA ALIE KARIBU KUJUA NINI KIMEWAPATA? AU HAWA SIO MASTAA? MAANA HATA PASSPORT UKIWA UGIRIKI UNANYIMWA AU AFISA ANAKWABIA SAFIRI NENDA ITALY SASA NITASAFIRI VIPI BILA HIYO PASSPORT?

    ReplyDelete
  7. Poleni vijana ndio kutafuta. Sasa jaribuni kutoa taarifa polisi hapo mlipo. Kisha chukueni ripoti ya kesi mkatafute Mwanasheria ambae atafungua kesi ya Wahanga wa makosa ya jinai. Hii itawezesha nyinyi kulipwa fidia. Msiache hiyo nafasi kama mnaishi kihalali hata kama ni mkimbizi uliyekuwa bado kwenye maombi. Hapo hamkosi kila mtu Euro 2000. Msiache hiyo nafasi na wala msiogope.

    ReplyDelete
  8. Anonymous wa kwanza nakupa pole sana kwa kukosa viza ya Marekani.

    ReplyDelete
  9. Ubalozi hawana lolote, wako busy kuwatafutia watoto wao maslahi na kupeleka magari etc etc bongo. Siwezi hata kusogea ubalozi, it is a waste of time.

    ReplyDelete
  10. Poleni ndugu zangu. Mungu awape roho ya uvumilivu na mpone. Swala la kurudi nyumbani siyo dawa ingawa Tanzania ni kwenu. Msichukue maamuzi yeyote ya haraka, muhimu sasa hivi ni kupata tiba na kuhakikisha kuwa afya zenu zinaimarika na pia usalama na amani yenu. Mungu awatunze, poleni sana.

    ReplyDelete
  11. Wizara ya Mambo ya nje tafadhali ingilieni kati suala hili. Ndugu zetu watanzania wengi hufanyiwa mambo ya kinyama sana huko nje. Hebu tusimame kama nchi kukemea suala hili, ingekuwa nchi za wajamaa zetu wa ASIA wangesha fika kwenye ubalozi wa nchi husika kwa vishindo.

    ReplyDelete
  12. Pamoja na changamoto lakini nyumbani ni nyumbani, utakosa vyote lakini hutakosa faraja toka kwa ndugu na jamaa. Kurudi sio suluhisho ila ndugu zetu mlio ughaibuni muwe waangalifu maana nyinyi ni kioo cha nchi yet jamani.

    ReplyDelete
  13. Serikali au wizard husika lazima iingilie kati kwani damu ya mtanzania haiwezi endelea kumwagika Kila kona ya dunia wakati nyie mpo.Watanzania wanaweza kulipiza kisasi kwa kuwadhuru watu wageni waliojaa nchini kwetu,ambapo sio kitu kizuri ila binadamu anapo kuwa helpless he can do anything to fight back.Haki lazima itendeke kumlinda Mtanzania na kumuheshimu popote pale Duniani.

    ReplyDelete
  14. Utawasaidiaje hao hata kama wewe ndiye ungekuwa balozi , wao wamejilipua wakijifanya WAKONGO sasa ana matatizo wanajiita WA Tanzania , rudini nyumbani tujenge Nchi huko hakufai hamchagui Nchi za kwenda nanyi? Ugiriki kuna nini/ pimeni kwanza mafanikio yenu mlopata mkiwa huko kama vipi njooni mwanerumango huku raha tupu.

    ReplyDelete
  15. Pole ndugu,
    Waswahili tunasema Akufukuzaye akwambii Toka,
    Ebu njoo ya ulaya ndo hayo Huku bado kuna amani ila nafahamu kuna mtu yupo hapo na ni Balozi wetu ebu muulizeeni Kazi ya ubalozi ni nini kama hawapi ushirikiano tembea kwamakundi Raisi amekataza watanzania kuonewa piga nanyinyi hatuwezi watu wetu wapigwe hata kuhuwawa ivivi Ebu msijilegeze Yangu ndo hayo

    ReplyDelete
  16. Poleni sana. Mungu atawaponya!

    ReplyDelete
  17. Inaweza kuwa ajali kazini(ktk kutafuta) lakini hapana budi kufuata sheria na taratibu, pia bima inasaidiaga.Dunia iko kama mzinga wa nyuki,walio ndani wanataka kutoka na walio nje wanataka kuingia. Hakika Bongo ni pazuri kuishi kuliko ughaibuni ambako wengi wakiona mweusi wanamshtukia shtukia kwa ubaya.

    ReplyDelete
  18. POLENI SANA NDUGU,TUNASIKITIKA MPAKA SASA HIVI BALOZI WETU KULE UGIRIKI HAJATOA TAARIFA YOYOTE KUHUSIANA NA HILI JANGA.JAMANI KAZI ZA BALOZI NJE YA NCHI MOJAWAPO NI KUWALINDA NA KUTETEA HAKI ZA WATANZANIA.MDAU GREATER LONDON.

    ReplyDelete
  19. Kama mpo kihalali ubalozi una haki ya kuwashughulikia lakini kama kujilipua mlie tu!!!!

    ReplyDelete
  20. hawa ni ndugu zetu na wote wapo kihalali Salum ana makaratasi ya Kudumu (permanent resident)na Said ana temporary , na wote wana uraia wa Tanzania ila hakuna hata balozi wa Tanzania Ugiriki balozi wa karibu ni Italy ambae wanaona wao kama vile ule msaada kukupatia kama huna haki vile na wao sio kazi yao.

    Mimi mwenyewe nimeishi Ugiriki kihalali na bado naendelea kutumia karatasi za kigiriki hapa London na huyo mmoja ni ndugu yangu wa Baba Mmoja Mama Mmoja ,nina bima ya kutosha huko Greece lakini Je hayo matibabu yapo?

    Kwa taarifa za leo ni kuwa Wameshaitwa Polisi kuwatambua Waliowapiga lakini kila kituo wakienda wanaambiwa nendeni kule nendeni kituo hiki yaani hakuna msaada kwa hao polisi pia.

    Suala la Nyumbani makaazi ni popote tu hata huko nyumbani kila siku watu wanachomwa kuuliwa acid yote hayo ni jumla ya matukio kwa hiyo bahati mbaya ni popote tu.

    Na watu wasifikiri kila mtanzania alieko nje ni mkimbizi hizo ni imani mbovu za kizamani sio .

    Suala je hao mabalozi au wizara zitashuhulika nao watu hawa au ndio hadi wawe mastar ? au wauza unga tu ndio wanashuhulikiwa tena wanawake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...