Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe
amewapokea Mabilionea 26 wa taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakiwa na wenza wao katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.
Mabilionea
hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama
sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda,
Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.
Katika
hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake, Prof. Maghembe
aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza "hakuna eneo lolote katika
uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores)
na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti".
Prof.
Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa
inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao
wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye amani na vivutio
vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea
Tanzania mapato.
Aidha,
aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi
unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.
(SOURCE: WWW.WIZARAYAMALIASILINAUTALII.BLOGSPOT.COM).
(SOURCE: WWW.WIZARAYAMALIASILINAUTALII.BLOGSPOT.COM).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi.
Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakimsikiliza Waziri Maghembe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...