Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewahukumu raia wawili wa India kutumikia kifungo cha kwenda jela miaka miwili ama kulipa faini ya Sh.milioni 64.

Hukumu hiyo ni baada ya kukiri mashtaka saba yaliyokuwa yakiwakabili likiwemo la kuipatia Serikali hasara ya zaidi ya Sh.milioni  694.

Mahakama pia imewaamuru wafungwa hao Kalrav Patel na Kamal Ashar kulipa Sh.milioni 694 ambazo waliisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA).

 Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa huku hiyo leo ambapo amesema mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao katika makosa saba ya uhujumu uchumi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amesema katika kosa la kwanza la kula njama, washtakiwa wanahukumiwa kwenda jela miezi 12 ama kulipa faini ya Sh.milioni 2 kwa kila mmoja.

Aidha katika kosa la pili hadi la saba, Hakimu Mashauri amesema wafungwa  hao  wamehukumiwa kwenda jela miaka 2 ama kulipa faini ya Sh.milioni 5 kwenye kila kosa kwa kila mshtakiwa.

Pia Mahakama hiyo imesema vyombo vyote ambavyo wafungwa hao walivitumia katika kuingilia miundombinu ya TCRA vimetaifishwa na Serikali.

Pia imeelezwa wakiwa maeneo ya Dar es Salaam na Zanzibar walikula njama ya kutaka kusafirisha vifaa vya mawasiliano bila kibali.

Ilidaiwa katika kipindi hicho mwaka 2015, washtakiwa hao walisafirisha vifaa vya mawasiliano kinyume na sheria za TCRA .

Mbali na mashtaka hayo pia wanakabiliwa na shtaka la kuingiza, kusimika nchini kifaa cha mawasiliano aina ya Voice Over internet protocol (Coop) na kukitumia bila ya kuthibishwa, na kusababisha hasara ya Sh.mil 694 kwa TCRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...