WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawachukulia hatua watendaji wote watakaobainika kuhujumu ujenzi wa miradi ya maji mkoani Mara.

Hatua hiyo imetokana na kutoridhishwa na utekelezwaji wa ujenzi miradi ya maji katika baadhi ya halmashauri za mkoa huo,hivyo kuwacheleweshea wananchi kupata huduma hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Januari 16, 2018) wakati alipokagua mradi wa maji wa Utegi uliopo katika kijiji cha Mika wilayani Rorya.Amesema Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo. Kampeni hiyo inalenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Waziri Mkuu amesema malengo ya kampeni hiyo ni kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.“Nitafuatilia katika maeneo yote ili kujua kama kiasi cha fedha kilichotolewa kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maji kinalingana na thamani halisi ya miradi husika.”

Waziri Mkuu amesema anakerwa na Halmashauri ya wilaya ya Rorya kutosimamia vizuri miradi ya maji inayotekelezwa katika wilaya hiyo, ikiwa ni pamoja na kutozingatia sheria.Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya wanaoshi wilayani Tarime wawe wamehamie Rorya ifikapo Februari 15, 2018.

“Atakayeng’ang’ania kuishi Tarime hadi siku hiyo atakuwa amejiondoa kazini mwenyewe. Lazima watumishi wote waishi kwenye vituo vyao vya kazi Rorya ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.”

Pia Waziri Mkuu aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutojihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo ulimaji wa bangi pamoja na uvuvi haramu na badala yake wafanye shughuli halali za kuwaingizia vipato.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 16, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Nati Hassan mmoja wa wazazi waliojifungua wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Kinesi wilayani Rorya Januari 16, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua Kituo cha Afya cha Kinesi wilayani Rorya Januari 16, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Nyamungo wilayani Rorya, Juma Wilfred baada ya kuzungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kinesi Januari 16, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Kituo cha wilaya cha Kipolisi cha Kinesi wilayani Rorya, SSP Juma Wilfred Majula (wapili kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho na kuvutiwa na juhudi ziizofanywa na Mkuu huyo wa Polisi za kujenga kituo hicho bila kusubiri fedha za serikali Januari 16, 201.. Waziri Mkuu aliendesha harambee ya papo kwa papo na kufanikiwa kupata shilingi milioni 20 za kumalizia jengo jipya la kituo hicho. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Tarime na Rorya, David Mwaibambe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Utegi wilayani Rorya wakati alipolazimika kuasimama baada ya kuona umati mkubwa watu waliokuwa na shauku ya kumuona na kuksikiliza Januari 16, 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...